

Kiungo Said Khamis Ndemla amesema kwa takribani wiki moja amekuwa akisumbuliwa na maradhi na anaendelea na matibabu nyumbani
Kiungo huyo ambaye mkataba wake na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu, anahusishwa kutaka kuondoka Simba
Tayari tetesi zinazomuhusisha kusajiliwa na Yanga zimeanza kushika kasi huku mwenyewe akisisitiza bado ni mchezaji halali wa Simba na angependa kusalia katika timu hiyo
"Mkataba wangu unamalizika mwishoni mwa msimu, sina haraka ya kusaini mkataba mpya na Simba kwani bado nasubiri nafasi ya kwenda kucheza soka nje ya nchi," amesema Ndemla
Ikumbukwe Ndemla alifanya majaribio katika klabu ya Eskilstuna ya Sweden na inaelezwa alifuzu majaribio hayo kinachosubiriwa ni yeye kuitwa kwenda kujiunga na timu hiyo
Hata hivyo amesema kama hilo halitatokea basi ataongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Simba
"Tetesi zote ambazo zimekuwa zikisemwa juu yangu naweza kusema zitabaki kuwa tetesi ila mipango kamili naijua mwenyewe, japo nasikia kuna watu wanazusha eti kuwa nilitolewa kambini kisa niligoma kusaini Simba, hilo si kweli, mimi ninaumwa sasa ni wiki nipo tu nyumbani naendelea na matibabu"



0 Comments