

TP Mazembe iliachana na mpango wa kumsajili kiungo wa Yanga Ibrahim Ajib baada ya mchezaji huyo kutaka kiasi kikubwa cha fedha za usajili, imefahamika
Inaelezwa TP Mazembe ilitaka kumsajili Ajib kwa dau la Dola 30,000 ambazo ni karibu Tsh Mil 70 za Kitanzania na mshahara wa Dola 3,000 ambazo ni zaidi ya Tsh Mil 7 kwa mwezi
Hata hivyo Ajib alitaka alipwe Dola 100,000 ambazo ni zaidi ya Tsh Mil 230 na mshahara wa Dola 5,000 ambazo ni zaidi ya Tsh Mil 10 kwa mwezi
Kinara huyo wa pasi za mabao ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu, anahusishwa kurejea timu yake ya zamani Simba lakini huenda akalazimika kukubali kupokea dau dogo zaidi ya hilo alilokataa TP Mazembe
Wakati huohuo inaelezwa kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amemuondoa Ajib katika mipango yake ya msimu ujao baada ya mchezaji huyo kukosa msimamo
Licha ya Ajib kuwasiliana na uongozi wa Yanga kutaka kufahamu mustakabali wa mkataba mpya, viongozi wamempa baraka zote akajiunge na timu anayotaka kwa kuwa hayuko kwenye mipango ya Zahera msimu ujao
Inaelezwa viongozi hao wanazo taarifa kuwa Ajib tayari amesaini mkataba wa awali klabu ya Simba



0 Comments