Kiungo mshambuliaji Issa Bigirimana ameomba kusitisha mkataba wake na klabu ya Yanga
Taarifa zilizopatikana mapema leo zimebainisha kuwa Bigirimana ameomba kuachwa ili akaendeleze maisha yake ya soka mahali pengine
Bigirimana ni mmoja wa wachezaji ambao walikuwa kwenye mpango wa 'kutemwa' dirisha dogo baada ya kushindwa kuonyesha makali yake tangu atue Yanga
Majeruhi ya mara kwa mara yamekuwa sababu kwake kutopata kabisa nafasi kwenye kikosi cha Yanga
Tayari Yanga imeachana na washambuliaji Sadney Urikhob na Juma Balinya ambao waliomba mikataba yao ivunjwe
Bila shaka Bigirimana pamoja na majeruhi Maybin Kalengo wako katika mkondo huo
0 Comments