Windows

Usajili wetu ni wa 'kimkakati' - Dk Ruhago




Uongozi wa Yanga umewatoa hofu mashabiki wake kuwa usajili unaofanyika sasa una lengo la kumaliza changamoto zote zilizojitokeza katika kikosi chao

Mapema leo Yanga ilitambulisha usajili wa mlinzi wa kushoto Adeyum Ahmed Saleh aliyetua kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya JKT Tanzania

Katibu Mkuu wa Yanga Dk David Ruhago alisema usajili wa nyota huyo umefanywa kwa kuzingatia mahitaji ya timu

"Usajili tunaofanya sasa ni maalum, ndio maana tuko makini sana. Wachezaji tunaowaleta sasa wanakuja kutatua changamoto zilizojitokeza," alisema

Adeyum anakuwa mchezaji wa pili kutua Yanga dirisha dogo baada ya mabingwa hao wa kihistoria kukamilisha usajili wa mshambuliaji Tariq Ismail Kiakala

Yanga pia tayari imemsajili mshambuliaji Ditram Nchimbi ambaye anasubiri kutambulishwa

Mashabiki wawataka Niyonzima, Miquissone

Wakati uongozi wa Yanga ukitumia utaratibu wa kutambulisha mchezaji mmoja mmoja, mashabiki wamekuwa na shauku ya kusikia utambulisho wa kiungo Haruna Niyonzima au mshambuliaji Luis Miquissone

Kuna taarifa kuwa Yanga imewasajili nyota hao wote wawili na kinachosubiriwa ni utambulisho

Afisa Mhamasishaji Antonio Nugaz amekataa kuthibitisha ujio wa nyota hao akiwataka mashabiki wafuatilie taarifa zinazotolewa na Yanga

"Wiki hii tutakuwa tukitambulisha mchezaji mmoja kila siku. Hadi kufikia Jumanne tutakuwa tumemaliza. Mashabiki waendelee kutufuatilia, wachezaji wote tuliowasajili tutawaweka hadharani"

Post a Comment

0 Comments