Windows

Azam: Tutapindua meza kibabe Zimbabwe

IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa hawana mashaka na maandalizi ya kikosi chao, wana imani ya kupindua meza kibabe Zimbabwe.

 

Azam FC itamenyana na Triangle United Septemba 28 mchezo wa marudio Hatua ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa jijini Bulawayo wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Azam Complex.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Cheche ambaye ni kiongozi wa msafara wa kwanza uliokwea pipa jana kuelekea nchini Zimbabwe, alisema kuwa wanajiamini na wamefanyia kazi makosa yao.

 

“Mpira wa sasa upo wazi na kila mmoja ana nafasi ya kushinda endapo atajiandaa vema, tunatambua kwamba mchezo wa kwanza tulipoteza nasi tunahitaji kurejea nyumbani na ushindi kama ambavyo wao walifanya,” alisema.

 

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

The post Azam: Tutapindua meza kibabe Zimbabwe appeared first on Global Publishers.


Post a Comment

0 Comments