Windows

Waziri Ummy atembelewa na Balozi wa Denmark


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametembelewa na Balozi wa Denmark nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Bw. Einar Jensen kwa lengo la kumuaga.

Waziri Ummy amemshukuru Balozi Jensen kwa kufanya kazi karibu na Wizara ya Afya na kusaidia kuboresha sekta ya afya ambapo hivi karibuni Balozi huyo alipata gawio toka Benki ya CRDB kiasi cha Tsh. Bilioni 6.7 na akaelekeza fedha hizo zitumike katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Kwa upande wake balozi huyo, amemshukuru Waziri Ummy kwa kuonesha ushirikiano katika kipindi chote alichofanya kazi hapa nchini huku akisifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuboresha maisha ya Watanzania hususani katika kuimarisha sekta ya afya ambayo ndiyo muhimili mkubwa wa maendeleo. Balozi Jensen amesema kama hakuna Afya hakuna maendeleo.


Post a Comment

0 Comments