Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, imefanikiwa kukamata kilo 300 za Dawa za Kulevya aina ya mirungi ambayo ilikuwa ikisafirishwa kwenda nchi za Ulaya hasa Uingereza ikidaiwa kuwa ni majani ya mronge.
Nyingine zimeandikwa kwa majina bandia ili zitambulike kama majani ya ‘morning tea’, ‘morning tea’, ‘tea leaves’, dawa za asili na majani ya mboga.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa Intelijensia wa mamlaka hiyo, Fredrick Kibuta, wakati akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam ambapo amesema katika tukio hilo watuhumiwa wawili ambao majina yao yamefichwa kwa uchunguzi zaidi wapo mbaroni.
Amesema kwa kushirikiana na Shirika la Posta, Wizara ya Kilimo na Mifugo, Wizara ya Maliasili na Utalii wamefanikiwa kukamata kilo hizo kwenye vifurushi vilivyokuwa vikiingizwa nchini kwa njia ya Posta kwenda nchi za Ulaya.
Amesema vifurushi hivyo vilikuwa vikitumia majina bandia ambapo uchunguzi wa kimaabara wa Mkemia Mkuu wa Serikali umethibitisha majani hayo yana kemikali Aina ya Cathinone ambayo inapatikana kwenye mmea was mrungi.
“Kuna taarifa ya uwepo wa usafirishaji wa kiasi kikubwa wa dawa za kulevya kutoka nchini kwenda nchi za Ulaya kwa njia ya Posta ambapo ilibainika dawa hizo zikiingizwa nchini kutoka nchini Ethiopia kama majani ya mronge kisha kufungwa tena na kwenda nchi za Ulaya, “amesema Kibuta.
0 Comments