Na Rahel Nyabali, Tabora
Waziri wa nchi tawala za mikoa na serikali za mitaa Suleiman Jafo amefanya uzinduzi wa kitaifa wa shule shikizi nchini.
Akizindua shule hizo kitaifa katika wilaya za nzega na Igunga mkoani Tabora ambazo zimejengwa kwa ufadhili wa shirika la maendeleo la kimataifa DFID Kupitia program ya eguipt,
Waziri Jafo amesema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi amepongeza mkoa wa Tabora kuwa miongoni mwa mikoa iliyofanya vizuri katika usimamizi wa miradi inaotekelezwa katika mikoa tisa hapa nchini. na kueleza namna serikali ilivyoridhishwa na matumizi ya fedha kiasi cha sh billion mia sita za program ya maboresho ya elimu nchini EQUIPT.
Awali Waziri Jafo pia alitembelea miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa ufugaji mbuzi katika shule ya msingi isimba na mradi wa ufugaji samaki katika shule ya msingi simbo ambayo inafadhiliwa na DFID.
Mkuu wa wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amasema Upatikanaji wa shule hizi utasaidia kuongeza ufauru kwa wanafunzi kwa kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni huku mwakilishi wa shirika la DFID Elizabeth Arthy akibainisha kuwa shirika hilo limetenga kiasi cha sh billion mia sita katika utekelezaji wa miradi hiyo.
0 Comments