MSANII wa Kike anayefanya vizuri sana kwenye game ya Bongo fleva, Mimi Mars leo amefanya mahojiano na kipindi cha BONGO 255 kinachoruka hewani kupitia + 255 Global Radio.
Mimi Mars ambaye ni mdogo wake Vanessa Mdee amezungumza mengi kuhusiana na kazi zake za Muziki, Maisha yake na mipango yake ya mbele katika tasnia nzima ya Bongofleva.
Ukiachana na Story za maisha yake na kazi zake ambazo zinafanya vizuri sana Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania, amegusia pia kuhusu sakata la Filamu ya The Lion King ambayo imezua gumzo sana Afrika Mashariki hasa baada ya wasanii wa Afrika Mashariki kutokushirikishwa katika Filamu hiyo.
Mimi Mars amesema “Sitoiangalia Filamu hiyo ikitoka kwa sababu wamenidisappoint sana. Haiwezekani Filamu iwe na maudhui ya Afrika mashariki halafu ukachukue wasanii wa Nigeria ..”
Kuhusu Mahusiano ya Vanessa na Jux kuvunjika, Mimi amesema kuwa mahusiano hayo ya dada yake yamempa funzo kubwa, na kusema kuwa hatokaa awe na mahusiano na mtu maarufu, kwa sababu ameona tension iliyokuwepo kwenye mahusiano ya dada yake na kuongeza kuwa mahusiano yake hatoyaweka hadharani.
Pia amefunguka kuhusu kumzimia sana msanii Mr. Blue na kuongeza kuwa alianza kumpenda Blue kitambo sana na anatamani sana kufanya naye kazi hata moja.
Tazama Video ya Interview nzima Hapa chini
The post Mahusiano ya Vanessa na Jux yamenipa Funzo (Picha + Video) appeared first on Global Publishers.
0 Comments