Windows

Kocha wa Simba SC kutumia mifumo mitatu msimu ujao


Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick Aussems amesema anataka kuona wachezaji wake wakicheza zaidi ya nafasi moja uwanjani kwani anataka kutumia mifumo zaidi miwili.

Patrick Aussems amesema hayo baada ya mchezo wa jana dhidi ya Platinum Stars ambao Simba SC iliibuka na ushindi wa magoli 4-1.

“Kwasasa nataka kuona wachezaji wakicheza nafasi zaidi ya moja sababu huu msimu nataka kuwa na mifumo miwili au mitatu” amesema.

Kwa sasa kikosi cha Simba SC kipo mjini Rusternburg nchini Afrika Kusini ambako kimeweka kambi kujiandaa na msimu mpya wa Ligi.



Post a Comment

0 Comments