Windows

Usajili wa ‘kishindo’ raha tupu Jangwani



WAKATI matajiri wa Yanga wakionekana kuwa makini na usajili msimu huu, kwa upande wa kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, ameonekana ni mwenye furaha na amani.

Iko hivi, Zahera kwa sasa hana presha huku akiendelea na majukumu yake na timu ya taifa ya DR Congo ambayo inajifua kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon), itakayofanyika nchini Misri mwezi huu.

Akiwa nchini humo na baadaye Misri, Zahera ataendelea kupewa taarifa za usajili unaoendelea Jangwani, ambako tayari Yanga wameshasainisha vifaa visivyopungua sita kutoka ndani na wale wa kimataifa.

Miongoni mwa wachezaji hao ni Abdul Azizi Makame (Zanzibar) na Farouk Shikalo (Kenya).

Kwa mujibu wa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo, Raoul Jean-Pierre Shungu, aliliambia BINGWA kuwa Zahera ameingia nchini humo tangu Jumanne na juzi wameanza safari ya kwenda Misri.

“Timu yetu ya Taifa inatarajia kuondoka kesho (juzi) kwa ajili ya Afcon na tayari Zahera tupo naye kwenye msafara huo,” alisema Shungu.

Awali Zahera alifunguka kuwa anahitaji kufanya usajili wa kibabe mapema kabla ya kuelekea kwenye michuano hiyo kwa sababu akiwa huko akili yake itahitaji utulivu wa hali ya juu.

“Namaliza kila kitu kabla ya kwenda Misri nikienda huko sitaki mawazo ya tofauti na kilichonipeleka,” alisema Zahera.

Post a Comment

0 Comments