

Uongozi wa Simba umesema usajili unaofanywa na timu hiyo unafuata mapendekezo ya kocha Mkuu Patrick Aussems na sio vinginevyo
Simba inaendelea kutambulisha wachezaji waliosaini mikataba ya kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara ambapo kila siku inatambulisha mchezaji mmoja
Mpaka sasa Simba imetambulisha wachezaji wapya wawili, mlinda lango Beno Kakolanya na beki Kennedy Wilson Juma ambaye hata hivyo usajili wake umeonekana kukosolewa na baadhi ya mashabiki
"Tuko makini sana kwenye usajili, hatusajili hovyo hovyo kwani tuna muongozo tulioachiwa na Mwalimu," amesema Mtendaji wa Simba Crescentius Magori
"Wachezaji wapya ambao tunawatambulisha tumejiridhisha wataweza kutusaidia kwenye michuano mbalimbali tutakayoshiriki msimu ujao"
"Zoezi la usajili linaendelea, mashabiki wetu wasiwe na wasiwasi tutaendelea kutambulisha wachezaji wapya kwa utaratibu wetu tuliojiwekea"
Pamoja na wachezaji hao wapya, wengine walioongeza mikataba ni John Bocco, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Jonas Mkude na Meddie Kagere
Zoezi la utambulisho linaendelea leo saa saba mchana



0 Comments