Boateng amesema alifanya ujinga mkubwa kununua gari tatu kwa siku moja ili apate furaha enzi zile akiwa Tottenham.
Kiungo huyo, ambaye sasa anaichezea Fiorentina, aliichezea Spurs kwa miaka miwili tangu 2007 hadi 2009 kabla hajaenda kwa mkopo Borussia Dortmund na baadaye kuuzwa Portsmouth.
Boateng, 32, aliichezea Tottenham mechi 14 tu kwa kipindi chote hicho huku akiweka wazi kuwa alikuwa mjinga na aliishi kama mfalme.
Akifunguka hivi karibuni, Boateng alitaja sababu ya kushindwa kuonyesha makali yake uwanjani alipokuwa Tottenham.
“Sikuwa nauchukulia mpira kama kazi. Nilikuwa mjinga. Nilikuwa na kipaji lakini nilifanya mazoezi mara chache sana, saa moja tu uwanjani.
“Nilikuwa wa mwisho kufika na wa kwanza kuondoka ili niende nikajirushe na marafiki. Nilikuwa na pesa, niliishi kama mfalme.
“Nilinunua magari matatu kwa siku moja nilipokuwa Tottenham: Lamborghini, Hummer na Cadillac. Kwa vijana, nawaambia: ‘Huwezi kununua furaha’.
“Nilikuwa na matatizo ya kifamilia. Nilikuwa natafuta furaha kwa vitu vinavyoo nekana: gari inakupa furaha kwa wiki tu. Nilinunua tatu ili niwe na furaha kwa wiki tatu.”
Boateng alifukuzwa na Schalke mwaka 2015 kwa tuhuma za tabia mbaya baada ya kuripotiwa alipatikana akiwa anavuta sigara huku akiwa amelewa chakari.
Mwaka 2012, mke wake Melissa Satta alidai kuwa Boateng alikuwa akiumiaumia kwa kuwa anafanya mapenzi sana. Mrembo huyo alisema: “Anaumia mara kwa mara kwa sababu tunafanya mapenzi mara saba hadi kumi kwa wiki.”
The post Boateng Akiri Ujinga Kununua Gari Tatu Kwa Siku Moja appeared first on Global Publishers.
0 Comments