Windows

Ryan Moon ndiye anayenukia Msimbazi


Mshambuliaji wa Kaizer Chiefs Ryan Moon ndiye anayetajwa kuwa mbioni kujiunga na mabingwa wa Tanzania Bara Simba

Moon tayari ameshaaga kunako klabu ya Kaizer Chiefs na anasubiri mkataba wake umalizike kabisa Juni 30 ili aanze maisha ya soka sehemu nyingine

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, alijiunga na Chiefs kwa mkataba wa miaka mitatu huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja

Ameichezea Chiefs mechi 42, amefunga mabao sita na kutengeneza pasi moja ya bao

Alijiunga na timu hiyo akiwa na miaka 18

Ni mchezaji anaye-endelea kuimarika kutokana na umri wake bado kuwa mdogo

Bila shaka kama akisajiliwa ataongeza kitu kwenye safu ya ushambuliaji ya Simba

Post a Comment

0 Comments