

Kiungo Mghana James Kotei ni miongoni mwa wachezaji waliomaliza mikataba kunako klabu ya Simba na inaelezwa bado hajasaini mkataba mpya
Hivi karibuni kocha Patrick Aussems alikanusha taarifa zilizokuwa zimezagaa kuwa alipendekeza Kotei aachwe ambapo alisisitiza Kotei ni mchezaji muhimu kwenye kikosi chake na kuutaka uongozi wa Simba umpe mkataba mpya
Kotei ambaye kwa sasa yuko kwao Ghana amesema wakati anaondoka jijini Dar es salaa hakukuwa na mazungumzo ambayo yalifanyika juu ya mkataba mpya
"Niko likizo Ghana naendelea na mazoezi binafsi huku nikiwasikiliza viongozi wa Simba. Hakuna mazungumzo ambayo nimefanya nao mpaka sasa, sifahamu mipango yao hivyo nimeanzisha mazungumzo na timu nyingine" amesema
"Kipaumbele changu bado ni Simba hata nikifikia makubaliano na timu nyingine nitawataarifu kwani nimeishi nao vizuri sana"
Kotei amekuwa akihusishwa kuwaniwa na timu kadhaa ikiwemo Kaizer Chiefs inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini
Ni miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri kwenye kikosi cha Simba kilichotwaa ubingwa msimu uliomalizika
Hakuna shaka uongozi wa Simba utampa mkataba mpya



0 Comments