Windows

Simba yaibeba Tanzania michuano ya CAF



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa timu nne kutoka Tanzania zitashiriki michuano ya CAF msimu wa 2019/20, mbili ligi ya mabingwa na mbili kombe la Shirikisho

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa mapema leo na TFF, Simba na Yanga zitashiriki ligi ya mabingwa na Azam Fc na KMC zitashiriki kombe la Shirikisho

Tanzania imeongezewa nafasi za michuano ya CAF baada ya kushika nafasi ya 12 kuwa miongoni mwa timu zinazopewa nafasi na nne na Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF)

Timu zote zilizopata nafasi kushiriki michuano hiyo zimetakiwa kujisajili kabla ya Juni 30 2019

Mafanikio iliyopata Simba kwenye michuano hiyo msimu huu, yameinufaisha nchi kwa kuongezwa idadi ya timu kutoka mbili na kuwa nne

Post a Comment

0 Comments