Windows

Tunajivunia mafanikio yetu kuongeza idadi ya timu CAF - Mo


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba Mohammed Dewji 'Mo' amesema Wanasimba wanapaswa kujivunia mafanikio waliyopata msimu huu katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwani yameisaidia Tanzania kuongezwa timu za kushiriki michuano ya CAF msimu ujao

Baada ya tamko kutolewa mapema leo na TFF juu ya Taarifa ya Tanzania kuongezwa timu nne kwanye michuano ya CAF, wadau wamepongeza juhudi kubwa zilizofanywa na Simba kufika robo fainali ya michuano hiyo

"Tunajivunia kuwa sehemu ya kufanikisha nchi yetu kuingiza timu nne kwenye michuano ya kimataifa, na tutaendelea kupambana kuhakikisha tunapata mafanikio makubwa kimataifa kwa maslahi ya klabu na nchi yetu," amesema Mo

"Hongera kwa Wanasimba wote kwa kazi kubwa tuliyofanya, tunastahili pongezi"

Simba mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara watashiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika huku wakiwabeba mgongoni watani zao Yanga ambao nao watashiriki michuano hiyo baada ya kumaliza nafasi ya pili

Azam Fc iliyotwaa kombe la FA itashiriki kombe la Shirikisho sambamba na KMC iliyomaliza kwenye nafasi ya nne katika msimamo wa ligi

Post a Comment

0 Comments