Windows

benchi la ufundi Simba kuamua kambi ya pre-season



Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems yuko likizo pamoja na timu yake yote ya benchi la ufundi baada ya kumaliza msimu kwa mafanikio

Hata hivyo inaelezwa mwishoni mwa mwezi huu Aussems na timu yake watarejea 'mzigoni' ambapo Simba inakabiliwa na michuano ya kombe la Kagame itakayofanyika nchini Rwanda kuanzia Julai 07 mpaka Julai 21

Baada ya michuano hiyo Simba itaeleka moja kwa moja kambini ambapo benchi la Ufundi limeachiwa jukumu la kupendekeza wapi timu ikaweke kambi ingawa tayari Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji 'Mo' alidokeza kuwa msimu huu kambi inaweza kuwa Ureno au Marekani

Mwaka jana Simba iliweka kambi Uturuki, kambi ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa kwa kuwawezesha mabingwa hao wa Tanzania Bara kuanza msimu vizuri na kumaliza vizuri wakitetea ubingwa wao pamoja na kufika robo fainali ligi ya mabingwa

Post a Comment

0 Comments