Windows

Yanga yaalikwa kushiriki Kagame Cup



Leo ni siku nzuri kwa Yanga kwani baada ya kupata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao, imepata mwaliko mwingine wa kushiriki michuano ya kombe la Kagame itakayofanyika nchini Rwanda mwezi Julai

Awali Simba na Azam Fc pekee kutoka Tanzania ndizo zilipaswa kushiriki michuano hiyo inayoshirikisha mabingwa wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)

Azam Fc ilitwaa taji hilo msimu uliopita hivyo itashiriki kama mabingwa watetezi

Mbali na Yanga, timu nyingine zilizoalikwa ni AS Vita Club na DC Motema Pembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na ZESCO United kutoka Zambia

Hii ni fursa kwa Yanga kuanza mapema maandalizi ya michuano ya ligi ya mabingwa ambayo hatua ya awali itaanza mwanzoni mwa mwezi wa nane

Mwaka jana Yanga haikushiriki michuano hiyo kutokana na changamoto ya 'ukata'

Post a Comment

0 Comments