Windows

Maproo saba kuachwa Simba



Uongozi wa Simba uko kwenye michakato ya kukamilisha usajili ambapo jana ulimtambulisha kiungo wa kigeni kutoka Sudan Sharaf Eldin Shiboub aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja

Inaelezwa kuna nyota wengine wanne ambao tayari wako nchini kumalizana na mabingwa hao wa Tanzania Bara

Taarifa ambazo zimeripotiwa na baadhi ya magazeti leo zinadai Simba imeamua kuachana na 'maproo' saba ambapo miongoni mwao wamo viungo Haruna Niyonzima na James Kotei

Wengine ni Zana Coulibaly, Nicholas Gyan, Emmanuel Okwi, Juuko Murshid na Asante Kwasi

Nyota wa kigeni waliobaki ni Meddie Kagere, Clatous Chama na Paschal Wawa

Baadhi ya nyota wameachwa baada ya mikataba yao kumalizika huku wengine wakitupiwa virago kutokana na kutokidhi vigezo vinavyohitajika kuendelea kubaki Msimbazi

Kwa upande wa Okwi ni suala la maslahi, awali ilielezwa kuwa Mganda huyo atasaini mkataba mpya baada ya kumaliza michuano ya Afcon inayoanza leo huko Misricut

Aidha wachezaji ambao usajili wao umekamilika ni Beno Kakolanya, Sharif Eldin Shiboub, Miraji Athumani, Kennedy Juma na Ibrahim Ajib

Simba pia iko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mlinzi wa kati raia wa Brazil Gerson Viera pamoja na nyota wengine wawili wa kigeni ambao tayari wako jijini Dar es salaam kusaini mikataba

Mwenyekiti wa Simba Swedi Mkwabi amesema wachezaji wapya watakaosajiliwa na timu hiyo hawatazidi saba

Post a Comment

0 Comments