Windows

Manara azitaka timu zilizopata nafasi CAF zijipange


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amezitaka timu zilizopata nafasi kushiriki michuano ya CAF msimu ujao zijipange ili kuendeleza mafanikio yaliyoletwa na Simba msimu uliomalizika

Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) limethibitisha kuwa Tanzania imetimiza vigezo vya kuwa na timu nne kwenye michuano yake

Yanga na KMC zimepata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho hivyo kuungana na Simba na Azam Fc ambazo zilijihakikishia nafasi mbili za awali

"Mafanikio iliyopata Simba kwa kufika hatua ya robo fainali yamezibeba Yanga na KMC. Tunahitaji kulinda nafasi hizi nne, hivyo hatutarajii kuona timu yoyote inatolewa hatua ya awali," amesema Manara

Katika hatua nyingine, Manara amewashukia wale waliokuwa wakikosoa Bodi ya ligi na TFF kuhusu viporo bila ya kuangalia faida ambayo leo kila mmoja anaifurahia

"Mmeona faida ya vile viporo vya Simba? Mnajisikiaje kucheza ligi ya mabingwa kwa mbeleko yetu?," ameandika Manara katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
"Yupo wapi aliesema ligi yetu ni mbovu? Nani anaweza kunyoosha kidole 

kulikokosoa Shirikisho letu na viongozi wao ambao toka enzi na enzi hawakuwahi kuingiza timu nne kwenye mashindano ya CAF?"

Post a Comment

0 Comments