Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba hawana presha kabisa na usajili kutokana na ubora wa kikosi chao kilichomaliza msimu kwa mafanikio makubwa
Kuelekea maandalizi ya msimu mpya mabosi wa Simba tayari wameanza kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyoachwa na kocha Patrick Aussems ambaye ametaka kusajiliwa wachezaji angalau wanne kuongeza nguvu kwenye kikosi chake
Mganda Juma Bulinya anayechezea timu ya Polisi ni miongoni mwa wachezaji wanaokaribia kutua Msimbazi
Majuzi Patrick Gakumba aliiletea timu hiyo majembe matatu, Bulinya ni miongoni mwa wachezaji hao
Askari Polisi huyo alimaliza kinara wa ufungaji ligi kuu ya Uganda akiweka kambani mabao 19
Inaelezwa mazungumzo ya kumsajili mchezaji huyo yamekamilika na wakati wowote atasaini mkataba
0 Comments