Uongozi wa Yanga uko kwenye mchakato wa kusaka kocha msaidizi kujaza nafasi iliyokuwa wazi kwa muda inayokaimiwa na Noel Mwandila
Mchakato huo huenda ukaharakishwa baada ya timu hiyo kupata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao
Kocha wa Kagera Sugar Meckie Mexime ndiye anayepewa nafasi kubwa kuwa msaidizi wa Mwinyi Zahera
Mara kadhaa Yanga ilijaribu kumnasa Mexime bila ya mafanikio, kocha huyo anapendelea zaidi kuwa Kocha Mkuu
Yanga inasaka kocha Msaidizi mzawa ambaye analifahamu vyema soka la Tanzania
0 Comments