Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemkabidhi Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba Haji Manara kiasi cha shilingi milioni tatu kwa kutambua mchango wake katika uhamasishaji wa mashabiki kuingia uwanjani na kuupenda mpira
Manara amekuwa kinara wa uhamasishaji Simba na timu ya Taifa, mchango wake ulionekana sana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Katika michuano hiyo Simba iliweka rekodi ya kuujaza uwanja wa Taifa katika michezo yote iliyochezwa nyumbani
Juzi katika hafla ya Mo Simba Awards Makonda aliwazawadia fedha Tsh Milioni Moja kila mchezaji aliyeshinda tuzo
Mlinda lango Aishi Manula yeye alizawadiwa Tsh Milioni 10 kutokana na mchango wake mkubwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
0 Comments