Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amerejea kwao Ubelgiji kwa ajili ya mapumziko baada ya kumalizika msimu wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Aussems ameondoka akiwa ameacha ripoti ya maboresho ya kikosi chake tayari kwa mikikimikiki ya msimu ujao
Inaelezwa kwenye ripoti hiyo ambayo tayari imejadiliwa na Bodi ya Wakurugenzi Simba chini ya Mwenyekiti Mohammed Dewji 'Mo', Aussems ametaka kuongezwa kwa nyota wanne kwenye kikosi chake
Ripoti hiyo imetilia mkazo kuimarishwa kwa safu ya ulinzi pamoja na kuongeza nguvu sehemu ya kiungo na ushambuliaji
Pia amependekeza maboresho ya mazingira ya maandalizi ya timu ikiwemo kununuliwa kwa vifaa vya kisasa kwa ajili ya mazoezi huku akitaka kocha wa makipa Mwarami Mohammed kuongezewa ujuzi
Aidha ametaka kocha Msaidizi wa Simba Denis Kitambi apewe mkataba wa muda mrefu baada ya kuridhishwa na uwezo wake
Kitambi alijiunga Simba kwa kusaini mkataba wa muda mfupi wa miezi minne
Tayari Simba imeanza kuifanyia kazi ripoti hiyo iliyoachwa na Aussems ambapo michakato ya usajili imeanza
Inaelezwa Simba imekamilisha usajili wa kiungo wa Gor Mahia Francis Kahata na iko kwenye majadiliano na Patrick Gakumba wakala wa nyota wengine watatu
0 Comments