Windows

Zahera atambua mchango wa nyota wanaoachwa Yanga



Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amekataa kutaja majina ya wachezaji watakaoachwa na timu hiyo mpaka mchezo wa mwisho dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumanne, May 28 upite

Akihojiwa na UFM jana, Zahera alisema usajili wa nyota wapya nane wanaotarajiwa kutua Yanga unamaanisha kuna wachezaji wataachwa

"Hatuwezi kusema nani tutamuacha kwa sababu ligi bado haijamalizika. Kwa sasa tuseme wachezaji wote wanaweza kuachwa na wachezaji wote wanaweza kubaki," alisema Zahera

Aidha Zahera ametambua mchango wa wachezaji wote msimu huu kwani walijitolea kwa moyo wote kuitumikia timu licha ya kupitia changamoto ngumu

"Roho inauma na huwa nawaza kila siku sijui nianzie wapi na niishie wapi, lakini lazima tuwaache baadhi ya wachezaji ili kutengeneza kikosi kizuri kwa ajili ya ushindani"

"Mimi naondoka Mei 28 usiku, kwahiyo wachezaji wote tunaowasajili msimu huu tutawatangaza tarehe hiyo

"Wachezaji nane tayari wameshakubali, sita ni wa Kimataifa na wawili ni wa hapa ndani ukiona wapya wanaingia basi kuna wanaotoka nieleweke ivyo lakini siwezi kusema sasa muda ukifika itafahamika

Post a Comment

0 Comments