

Uongozi wa Simba umekiri kupokea ofa kutoka vilabu kadhaa vinavyowawania nyota wake mshambuliaji Meddie Kagere na kiungo Clatous Chama
Inaelezwa klabu ya Zamalek ndiyo iliyowasilisha ofa kumtaka Kagere
Vigogo hao wa soka barani Afrika wanaoshiriki ligi kuu ya Misri, wametuma ofa ya zaidi ya Tsh Milioni 900 kumtaka Kagere
Hiyo ni ofa ya pili kutumwa na Zamalek kwa Simba baada ya ofa ya kwanza ya Tsh Milioni 700 kupotezewa na uongozi wa Simba
Kagere akiwa kwenye msimu wake wa kwanza Simba, amekuwa na kiwango kizuri akiisaidia Simba kufika hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Kagere anaongoza kwa kupachika mabao ligi kuu ya Tanzania Bara akiwa amefunga mabao 23
Mtendaji wa Simba Crescentius Magori amesema wamewasiliana na timu mbili kutoka Arabuni zinazowawania nyota waocut
Magori amesema hawana lengo la kuwauza nyota wao lakini kama watapokea ofa nzuri basi wanaweza kuzungumza
Meneja wa Kagere Patrick Gakumba amesema Zamalek imedhamiria kumsajili Kagere lakini uamuzi wa mwisho uko mikononi mwa Simba inayommiliki mchezaji huyo
"Kagere ni mchezaji wa Simba bado yuko kwenye mkataba na timu hiyo, kimsingi Zamalek wanapaswa kumalizana na Simba," amesema



0 Comments