Jumanne, May 28 2019 ligi kuu ya Tanzania Bara itafika tamati kwa timu zote 20 zinazoshiriki ligi hiyo kushuka viwanjani
Kama ilivyokuwa msimu uliopita, Yanga inamaliza msimu kwa kuumana na Azam Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru
Mabingwa hao wa kihistoria watautumia mchezo huo kuwaaga baadhi ya nyota wake ambao hawatakuwa na timu hiyo msimu ujao
Mcongomani Heritier Makambo na Ibrahim Ajib tayari wameaga, wakitarajiwa kuondoka klabuni hapo baada ya mchezo huo
"Ajib na Makambo wataondoka baada ya mchezo dhidi ya Azam Fc. Tutautumia mchezo huo kuwaaga na kuwashukuru kwa mchango wao kwa timu yetu katika kipindi chote tulichokuwa nao," amesema Mratibu wa Yanga Hafidh Salehcut
Mbali na wachezaji hao, wapo wengine ambao mikataba yao inamalizika na hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema baada ya mchezo huo watawapa mkono wa kwa heri wachezaji wote ambao hawataendelea kuitumikia Yanga
Zahera amesema Yanga iko mbioni kukamilisha usajili wa wachezaji nane ambao wanachukua nafasi za wachezaji watakaoachwa
0 Comments