Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' juzi alikutana na wachezaji na benchi la ufundi la klabu hiyo
Katika kikao hicho, masuala mbalimbali yalijadilwa, lakini kubwa ni ahadi aliyoitoa kwa wachezaji kama watafanikiwa kutetea ubingwa
Mo ameahidi kutoa 'BONUS' ya Tsh Milioni tano kwa kila mchezaji kama watatwaa ubingwa
Baada ya kikao hicho, kikosi kiliingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Ndanda ambao utapigwa leo katika uwanja wa Uhuru
Ahadi hiyo imeongeza mzuka kwa wachezaji ambao sasa wamepania kushinda mchezo wa leo na ule unaofuata dhidi ya Singida United ili kujihakikishia 'mshiko' huo wa maana kutoka kwa boss 'Mo'
0 Comments