Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba leo wanashuka uwanja wa Uhuru kuikabili Ndanda Fc katika mchezo ambao matokeo ya ushindi yataisogeza Simba karibu ya ubingwa wa pili mfululizo
Simba inayoongoza ligi ikiwa na alama 85, inahitaji alama nne tu kutetea ubingwa kwa msimu wa pili
Kuhakikisha alama tatu zinapatikana leo, kikosi cha Simba kiliingia kambini juzi baada ya kufanya kikao na Mwekezaji wa klabu hiyo Bilionea Mohammed Dewji 'Mo'
Hesabu za kocha Patrick Aussems ni kuhakikisha wanashinda mchezo wa leo na ule utakaofuata dhidi ya Singida United ili kujihakikishia ubingwa kabla ya mechi mbili za mwisho
Baada ya mchezo leo, Simba itaondoka jijini Dar es salaam kuelekea Singida ambako keshokutwa Jumanne, May 21 itacheza na Singida Unitedcut
May 22 Simba itafunga safari kurejea jijini Dar es salaam ambapo May 23 inakabiliwa na mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Sevilla
Sevilla inatarajiwa kuwasili keshokutwa tayari kwa mchezo huo ambao utalipaisha jina la Simba na Tanzania Kimataifa kwani utarushwa 'mbashara' na vituo vikubwa vya runinga duniani
Kuelekea mchezo wa leo, Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema wachezaji wa timu hiyo wako tayari, wanafahamu Wanamsimbazi wanahitaji ushindi
0 Comments