Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema ataendelea kubaki timu hiyo licha ya timu kadhaa kumuwania
Akizungumza jana kwenye hafla ya Iftar Gala Dinner, Zahera amefichua mwishoni mwa mwaka jana klabu ya Buldcon ya Zambia ilimtumia ofa nono ili akajiunge nayo
Ikumbukwe Zahera ilikuwa ajiunge na klabu hiyo kabla ya kupigiwa simu na mdogo wake kuja kujiunga na Yanga siku ambayo alipaswa kusaini mkataba
"Mwezi 11, Buildcon walinipigia simu niende Zambia nikajiunge nao. Kocha Noel (Mwandila) anafahamu"
"Waliahidi kunilipa mshahara wa dola 15,000 (zaidi ya Tsh Milioni 34) lakini nikawaambia mimi nina mkataba na Yanga siwezi kuondoka"
ATAJA SABABU YA KUBAKI YANGA
Kocha Zahera amesema watu wengi wamekuwa wakimuuliza maswali kwa nini anabaki Yanga, timu yenye matatizo mengi?
Zahera amesema amepewa maono na Mungu kuwa yuko sehemu sahihi na anaamini matatizo haya yatamalizika
"Watu wengi wananiuliza, Coach kwa nini unan'gan'gania kubaki timu yenye matatizo?"
"Nimewaambia fedha sio kila kitu kwangu. Lakini pia mimi nimepewa maono na Mungu kuwa napaswa kuwa hapa"
"Naamini haya matatizo yataisha na timu hii itarejea pale inapostahili"
AWASIFU WACHEZAJI
Zahera amewasifu wachezaji wa Yanga kwa kujitolea kwao na kuipa mafanikio timu licha ya changamoto nyingi zilizowakabili msimu huu
"Naomba muwapigie makofi ya nguvu wachezaji wote. Wamefanya kazi kubwa"
"Naamini kama sio kudhurumiwa kwenye baadhi ya michezo, leo hii tumebaki na mechi mbili tungekuwa tunasherehekea ubingwa"
"Tumefanyiwa dhuruma katika michezo sita, isingekuwa hivyo, wachezaji hawa wangefanikiwa kuchukua ubingwa licha ya kucheza kwenye mazingira magumu sana"cut
ATAKA MASHABIKI VIWANJANI
Yanga imekumbwa na changamoto ya mashabiki wake kutojitokeza kwa wingi uwanjani licha ya timu hiyo kuwa na rekodi ya kipekee Tanzania
Zahera amesema ni wakati sasa vongozi kujiuliza kwa nini mashabiki hawafiki viwanjani
"Mini ninafahamu sababu, lakini nanyi mjiulize kwa nini mashabiki hawaji uwanjani?"
VIONGOZI WAPYA WAUNGWE MKONO
Kocha Zahera amewataka Wanayanga wote kuwaunga mkono viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni ili waweze kuipa mafanikio timu hiyo
Aidha Zahera amewapongeza viongozi waliopita kuwa walifanya kazi nzuri lakini walikwama kutokana na mazingira waliyokumbana nayo
"Viongozi waliopita hawakuwa wabaya, walifanya kazi kubwa lakini walikumbana na hali ngumu"
0 Comments