

Wakati Ligi Kuu ya Tanzania Bara ikielekea mwishoni Rais wa TFF Wallace Karia amezungumzia masuala mbalimbali na changamoto zilizoikabili ligi hiyo msimu huu kupitia mahojiano yake na kipindi cha SportsXtra
Baadhi ya mambo aliyoyaainisha;
LIGI KUU
Ligi inaelekea ukingoni, tunashukuru inaenda salama mbali ya changamoto chache zilizojitokeza hususan za waamuzi lakini kama shirikisho tutasimamia kuhakikisha waamuzi wanachezesha kwa haki
Vilabu vimetoa ushindani mkubwa kuna tafsiri tofauti kwamba vilabu vimejaa pamoja kwenye pointi gape lipo sawa ukiacha tatu za juu. Vilabu vingi vimejaa kwenye pointi 40+ hakuna timu yenye pointi 50, ni mazingira tu ya mashindano haya.
Mashindano yamekuwa ni mazuri timu zinashinda hata zikiwa ugenini kuna wakati ligi iligeuka ikawa vigumu timu kushinda ikiwa ugenini.
WAAMUZI
Tumeshakusanya takwimu za waamuzi wengi, msimu unaokuja tutawapunguza wengi sana tutabaki na cream ya waamuzi na tutawaweka kwenye madaraja. Anayefanya vizuri atapanda daraja asiyefanya vizuri atashuka.
VILABU SIO VINGI LIGI KUU
Nchi yetu ni kubwa na inamikoa mingi, hata kila mkoa ukiwa una timu moja ligi kuu kuna mikoa bado haitaweza kuingia ligi kuu kwa sababu idadi itakuwa kubwa.
Matamanio yangu ni kuona endapo mkoa unakosa timu ligi kuu basi uwe na timu daraja la kwanza au daraja la pili kwa sababu ndio ligi za juu kwa Tanzania.
KUPUNGUZA VILABU
Hatutapunguza vilabu ilimradi tu, tutakuwa wakali kwenye masharti ya club licencing na club licence itakapokuwa inafanya kazi vilabu vitaamua vyenyewe kutafuta rasilimali fedha na kujiendesha. Klabu isiyoweza kujiendesha itaondoka kwenye ligi na hakutakuwa na mbadala kwa hiyo tutakuwa tunazipunguza kutokana na kigezo cha club licencing.
WASILAUMU LIGI HAINA MDHAMINI
Viongozi wa timu wasiishie kulaumu ligi ngumu haina mdhamini wakati walikuwa wanacheza ligi daraja la pili na daraja la kwanza ambazo hazina udhamini na hawakulaumu, wamefika ligi kuu wanasema ligi haina mdhamini.
PROGRAM ZA VIJANA
Timu zote 20 za ligi kuu zikiwa na program za vijana Tanzania itapiga hatua lakini itawasaidia wenyewe kiuchumi, wachezaji hao watakapopata timu nyingine bila shaka watauzwa. Kwa hiyo vilabu vinapaswa kutambua kwamba vyenyewe ni viwanda na bidhaa zinazoweza kuwapatia fedha kuendesha klabu zao ni wachezaji vijana.



0 Comments