Windows

Ten ataja kinachojaza mashabiki uwanjani, ampiga dongo Manara 'kiaina


Kwa takribani misimu miwili idadi ya mashabiki wa soka wanaofika uwanjani hasa kwa klabu ya Yanga imekuwa ikipungua hali iliyopelekea kuibuka kwa mijadala miongoni mwa wadau
Miaka mitatu, minne nyuma Yanga ilikuwa inafahamika kwa kuwa na mashabiki wengi, walikuwa wakijitokeza kwa wingi uwanjani, lakini sio sasa
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Dismas Ten ametoa maoni yake juu kinachopelekea mashabiki kujitokeza uwanjani kwa wingi kushuhudia timu yao inapocheza
"Ninavyoamini mimi, mashabiki wa soka kwenda uwanjani ndiyo utamaduni halisi wa soka, ndiyo maana vilijengwa viwanja vya soka na si soka kuchezwa kwenye vituo vya daladala," Ten aliuambia mtandao wa mkalamangi
"Kitu muhimu ni klabu au timu kutengeneza mazingira mazuri ya kumfanya mtu kwenda uwanjani
"Kuwa na kikosi kizuri,imara chenye uhakika wa ushindi, wachezaji wazuri ambao ni brand, urahisi wa tiketi na usalama. Huwezi kusema kwamba ili watu waende uwanjani ni lazima kuunda kamati. So siku kamati isipokuwepo ina maana watu wasiende uwanjani hapana!
"Mimi siyo mmoja wa wanaomini kuwa makelele ya mtu au mtu kukashifu wengine ndo sababu ya watu kwenda uwanjani? haiwezi kuwa hivyo, siku mtu huyo asipokuwepo duniani? viwanja vifungwe? Big No
"Nijuavyo mapenzi kwa timu zao ndo kitu pekee kinachowapeleka watu kuziangalia zinapocheza..!
Ukiniambia leo kwamba watu wanaenda kwa sababu hiyo nitakuuliza kabla @fifa hawajatoa maelekezo ya kuwepo kwa nafasi hizi viwanjani kulikuwa hakuendi watu?
"Ni mara ngapi Uwanja wa Taifa ( sasa uhuru) ulijaa mashabiki kwa mechi za timu zetu kubwa kipindi hicho? Ni mara ngapi CCM Kirumba ilifurika mashabiki wakiitizama mechi ya PAMBA na USHIRIKA ya Moshi au Kambarage Stadium ikijaa kwa mechi ya Biashara Shinyanga na Sigara ya Dar es Salaam.
"Wakati huo wote hakukuwa na kamati wala kelele za mtu kabla ya mchezo
"Kwenda uwanjani ni utamaduni ambao watu wa soka wanapaswa kuishi nao," amesema Ten
cut
Kimsingi jambo muhimu hapa ni hili la ubora wa timu na mazingira rafiki yatakayowezesha mashabiki kwenda uwanjani, kwa kiasi kikubwa msemaji wa Yanga yuko sahihi
Mfano klabu ya Simba msimu huu mashabiki wake wamejitokeza kwa wingi uwanjani kutokana na timu yao kuwa bora na kufanya vizuri, hiyo ndio hamasa kubwa inayowafanya wajitokeze uwanjani kuliko 'kelele' za msemaji wao
Hata kama uhamasishaji mkubwa utafanyika halafu timu ikawa haifanyi vizuri mashabiki wataacha kwenda uwanjani.
Shabiki anapokwenda uwanjani anatarajia kurudi na furaha kwa timu yake kushinda, lakini ikitokea kila anapokwenda anarudi na maumivu itafika wakati ataacha
Hilo ndilo lililoikumba Yanga katika misimu hii miwili. Mashabiki wengi wamekata tamaa na timu yao
Bila shaka uongozi wa Yanga utaifanyia kazi changamoto hii kama walivyoahidi, kuboresha kikosi pamoja na kumaliza changamoto za kiuchumi zinazoikabili Yanga

Post a Comment

0 Comments