

Jumatano ijayo Yanga itashuka dimba la Uhuru kuikabili Mbeya City katika moja ya michezo miwili ya lala salama ligi kuu ya Tanzania Bara
Kikosi cha Yanga kinaendelea kujifua kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kikiwa chini ya kocha Msaidizi Noel Mwandila akitimiza majukumu aliyoachiwa na Mwinyi Zahera aliyesafiri nje ya nchi
Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema mazoezi ya timu hiyo yanaendelea vizuri, wana matumaini makubwa ya kumaliza vizuri ligi kwa kushinda michezo yote miwili iliyobaki
Mrisho Ngassa, Ibrahimu Ajib, Andrew Vicent, Juma Makapu na Heritier Makambo walikosa mazoezi ya jana jioni kutokana na sababu mbalimbali, wengine wakiwa wagonjwa huku wengine wakiwa na ruhusa
Makambo tayari amejiunga na Horoya AC ya Guinea
Kimahesabu Yanga bado imo katika kuwania ubingwa, mechi mbili zinazofuata za Simba zitabainisha hatma ya ubingwa kwa Yanga
Kama Simba itashinda michezo yote miwili dhidi ya Ndanda Fc na Singida United au itashinda mmoja na kupata sare mwingine, basi itajihakikishia kutwaa ubingwa na michezo iliyobaki ya Yanga itakuwa ya kukamilisha ratiba tu



0 Comments