Windows

Tetesi za Usajili Tanzania leo 9 May 2019

BEKI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Yakubu Mohammed, amesaini mkataba mpya wa miaka miwili leo alhamisi.

Awali mkataba wa Yakubu ulikuwa ukitarajia kumalizika Novemba mwaka huu, hivyo kwa kuongeza mkataba huo kutamfanya aendelea kuitumikia Azam FC hadi 2021.

Nyota huyo amekuwa na kiwango kizuri tokea ajiunge na Azam FC Novemba 2016, akitokea Aduana Stars ya Ghana, ambapo kwa mara ya kwanza alisaini mkataba wa miaka mitatu.

Beki huyo raia wa Ghana, amesaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin, Mratibu wa timu, Phillip Alando na Wakala wake, Joseph Epton.

The post Tetesi za Usajili Tanzania leo 9 May 2019 appeared first on KWATA UNIT SPORTS & ENTERTAINMENT.



Post a Comment

0 Comments