

Ni siku nyingine tena imepita, tumerudi salama majumbani mwetu, kuungana tena na wapendwa wetu, familia na watoto pia... Baadhi yetu hatujarejea, tuko mishe na viti virefu... Baadhi tuna sababu za msingi na nyumbani wanafahamu na tumewapa taarifa, wanatusubiri watupokee kwa upendo, kwa furaha kwa bashasha kuu
Baadhi hali ni tofauti, hatungependa kuchelewa nyumbani.... Tungependa tuwahi, tuungane na familia, tuimalize jioni kwa furaha kuu kabla hatujaungana kwa dinner na maombi ya usiku.... Lakini hali ni tofauti tunapoteza muda nje saa zisogee ili tukifika tu ni chakula kuoga na kulala... Tunakimbia kero na malumbano yasiyoisha
Ndoa haina furaha.... Ndoa haina amani, majuto ni mengi mno moyoni.. Kila mmoja anajutia kivyake... Hakuna upendo tena... Hakuna kuaminiana tena... Ni mwendo wa kutuhumiana na kuviziana....




Hakuna upendo, hakuna sharing, hakuna majadiliano ya changamoto, ya maumivu ya kushinda na kushindwa, ya kutiana moyo na kufarijiana... Kila mtu kivyake... Kila mtu na lwake...








Karibuni wanandoa wote.. Ni mada ya kupeana faraja na kushare maumivu... Itambueni nguvu ya kuongea... Kuongea hupunguza maumivu mengi... Kupitia mada hii utajiona hauko pekeyako na pengine utaona kuwa kumbe wewe una nafuu kubwa ukisikia ya mwenzako. Jisikie huru ufunguke....
Funguka kwenye ndoa yako iliyoumizwa na kujeruhiwa sana, iliyotiwa vidonda na makovu ya kila aina
Ya usaliti
Ya kuchapiwa
Ya kusingiziwa
Ya kunenewa mabaya
Ya kudharauliwa kutukanwa na kudhalilishwa
Funguka upate nafuu
Funguka upate faraja
Funguka upunguze sumu mwilini
Funguka upate kupona sasa....
Karibuni wanandoa wote



0 Comments