

Kikosi cha Yanga kinashuka dimbani kesho Karume Stadium mjini Musoma, Mara kucheza na Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Yanga inaenda kukipiga na Biashara ikiwa imeshushwa nafasi ya pili kunako msimamo wa ligi ikiwa na alama 80 dhidi ya 81 za Simba.
Kuelekea mchezo huo Yanga wamedhamiria kwa dhati kupata matokeo ili kushinda waweze kurejea tena kwenye nafasi ya kwanza.
Kwa utofauti wa alama uliopo Yanga ikishinda mchezo wa kesho itapanda tena mpaka nafasi ya kwanza na itafikisha alama 83 na kuwaacha Simba kwa alama mbili.
Hata hivyo Yanga itakosa huduma ya mchezaji wake Ibrahim Ajibu ambaye ameachwa Dar es Salaam kutokana na kuwa majeruhi.




0 Comments