Windows

RASMI YANGA YAMALIZANA NA KAKOLANYA


Ni kama mambo yameiva vile juu ya Yanga na kipa Beno Kakolanya ambapo taarifa zilizopo zinaeleza kuwa uongozi wa klabu yake umeamua kuachana naye rasmi.

Taarifa zinasema kuwa baada ya uongozi mpya kuingia madarakani chini ya Mwenyekiti wake Mshindo Msolla, umeamua kuketi chini na kufikia mwafaka wa kuachana na Kakolanya.

Ikimbukwe Kakolanya akiingia kwenye sintofahamu na Kocha wake Mwinyi Zahera mpaka kufikia hatua ya kumtema kikosini na mpaka sasa akawa hana timu ya kuchezea.

Kakolanya aligoma kuendelea na kazi Yanga kutokana na kutolipwa fedha zake za mshahara pamoja na za usajili hivyo kuamua kujiondoa mwenyewe kwa kuanza kugomea mechi.

Kuondoka kwa Kakolanya Yanga kunamfanya sasa awe huru na timu yoyote inaweza kumsajili hivi sasa.

Post a Comment

0 Comments