Windows

SIMBA YAPEWA RASMI UBINGWA LIGI KUU


Kutokana na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania jioni ya jana, unaambiwa mashabiki wengi wa timu ya Simba wamesema ubingwa wa ligi msimu huu utatua kwao.

Jeuri hiyo imekuja kutokana na ushindi huo uliowafanya kuifikishia Simba alama 72 huku watani zao wa jadi Yanga wakiwa na 77.

Wengi wameeleza kuwa kwa Simba hii ya sasa wana asilimia kubwa ya kutetea taji lao licha ya kuwa na mechi kadhaa ngumu zilizosalia ikiwemo ya Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar pia Azam FC.

Simba ilikuwa na viporo vingi kutokana na ushiriki wake wa mashindano ya kimataifa uliosababisha mechi zake za ligi kurundikana na mara baada ya kutolewa ilibidi waanze kuvicheza.

Mpaka sasa wekundu hao wa Msimbazi wamepoteza mechi mbili pekee msimu huu ikiwa ni dhidi ya Mbao FC na Kagera Sugar.

Post a Comment

0 Comments