Baadhi ya mashabiki na wanachama wa klabu ya Yanga wamelitupia lawama Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuipangia Simba kucheza na Sevilla ya Spain.
Hatua hiyo imekuja mara baaa ya TFF kuthibitisha kuwa Simba itakipiga na Sevila kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa kirafiki kuelekea msimu ujao.
Mashabiki na wanachama hao wamesema kuwa awali ilielezwa kulipaswa kufanyike mechi baina ya watani wa jadi ili mshindi ndiyo acheze na Sevilla.
TFF kwa kushirikiana na SportPesa wameamua kuwachagua Simba kucheza na Sevilla kwa kuangalia ubora wa miaka ya hivi karibuni.
Rekodi zinaonesha kuwa Simba ndiyo wamekuwa bora zaidi katika Ligi Kuu Bara kwa miaka ya hivi karibuni ukilinganisha na timu zingine.
0 Comments