Simba iliibuka na ushindi huo kupitia bao la Hassan Dilunga aliyefunga katika dakika ya mwisho kabisa zikiwa zimeongezwa hizo saba ambao zimeleta hoja kubwa haswa kwa mashabiki wa upande wa pili ambao ni Yanga.
Kupitia mitandao na hata vijiweni kumeonekana mashabiki wengi wa Yanga wakihoji imekuwaje mechi hiyo iongezewe dakika saba na wengi wao wakiamini hazikuwa zinastahili.
Asilimia kubwa wamesema kuwa ni kama kulikuwa na upendeleo wa kuitafutia Simba matokeo wakiamini mechi ilikuwa inamalizika kwa matokeo ya 0-0.
Malalamiko hayo yamekuja ikiwa Simba na Yanga zinawania ubingwa wa Ligi Kuu Bara huku wekundu hao wa Msimbazi wakiwa bado na viporo vya mechi wakielekea kuvikamilisha.
0 Comments