Simba inahitaji kushinda michezo minne tu ili iweze kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo
Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara amesema wanakusudia kuiomba TFF iwakabidhi kombe la ubingwa kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Sevilla utakaopigwa May 23 katika uwanja wa Taifa
Manara amesema wamejipanga kushinda michezo yote minne itakayopigwa kabla ya mchezo dhidi ya Sevilla ili kuhakikisha lengo lao linafanikiwa
"Tukishinda michezo minne inayofuata tutaweza kutetea ubingwa bila ya kujali matokeo ya wapinzani wetu"
"Tutawaomba TFF watukabidhi kombe siku ya mchezo na Sevilla ikiwapendeza, kwa kuwa huo ni mmoja wa mchezo mkubwa zaidi kuwahi kuchezwa nchini na itakuwa heshma kwa Shirikisho na soka letu kwa ujumla," amesema Manara
Simba inashuka uwanja wa Uhuru kesho kuikabili Kagera Sugar katika mchezo ambao mabingwa hao watakuwa na nafasi ya kulipa kisasi cha kipigo cha mabao 2-1 cha mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa mwezi uliopita

0 Comments