

Uongozi wa klabu ya Yanga leo umemalizana na aliyekuwa mlinda mlango wao namba moja Beno Kakolanya na sasa mchezaji huyo yupo huru kujiunga na timu yoyote.
Kakolanya amekuwa nje ya uwanja kwa karibia msimu mzima baada ya kugoma kuichezea timu hiyo ili kushinikiza kulipwa stahiki zake hali iliyopelekea kutofautiana na kocha mkuu Mwinyi Zahera ambaye aliamua kuachana nae.
Uongozi wa Yanga umempa Mwanasheria wa mchezaji huyo, Leonard Richard barua ya kuachana leo asubuhi na kumfanya nyota huyo wa zamani wa Tanzania Prisons kuwa huru kujiunga na timu yoyote kuanzia sasa.
Kakolanya ameiambia wapendasoka kuwa amefurahi suala hilo kumalizika huku akiziita mezani timu zinazohitaji huduma yake ili aweze kurejea dimbani. “Leo nimepokea barua kutoka Yanga ya kumalizana kwa amani tu, namshukuru Mungu sasa nipo huru na ninaweza kujiunga na timu yoyote ambayo tutafikia makubaliano,” alisema Kakolanya.
credit : Wapenda Soka
The post Maamuzi ya mwisho yafikiwa kati ya Beno na Yanga leo appeared first on KWATA UNIT SPORTS & ENTERTAINMENT.



0 Comments