Windows

Samatta anafunga tu Ulaya






MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameendelea kuwa tishio Ulaya baada ya juzi kufunga tena katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Belgium akiwa na klabu yake ya Genk.

Juzi Genk ilipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Royal Antwerp katika mchezo wa kumtafuta Bingwa wa Ligi hiyo ambayo kwa sasa zipo timu sita katika kundi moja ambalo litaamulu Bingwa wa msimu huu, baada ya michezo ya nyumbani na ugenini.

Samatta alifunga bao hilo dakika ya 55 baada ya beki wa timu pinzani kufanya makosa ya kumpa mpira bila kufanya makosa nyota huyo waTaifa Stars aliandika bao dakika za mwanzo kipindi cha pili.

Ni wazi kuwa ufungaji bora kwa mchezaji huyo unamnyemelea kutokana na idadi ya magoli 23 aliyonayo hivyo kumuacha mpinzani wake Harbaoui Hamdi akiwa na magoli 18 na kuwaacha mbali wanaofuatia huku ikiwa imebaki michezo mitatu kabla ya Ligi hiyo kumalizika.

Ligi hiyo ilimalizika kwa Genk ikiongoza kwa pointi 63, hivyo timu sita kuingia katika hatua ya Play off inayoshirikisha timu sita kulingana na msimamo wa Ligi kwa ajili ya kumtafua bingwa mpya wa msimu huku pointi za kila timu zikigawanywa kwa mbili kabla ya hatua hiyo.

Katika hatua hiyo kuna timu za Genk, Standard Liege, Anderlecht, Anterwap, Club Brugge na Gent ambazo zinasaka ubingwa huo licha ya Genk ya Samatta kumaliza nafasi ya juu.

Katika Sheria ya Ligi hiyo ambayo inashirikisha timu 16 kwa maana kila timu inacheza michezo 30, baada ya Ligi kuisha timu sita za juu zinaingia katika hatua ya playoff kutafutwa bingwa na baada ya hapo atakayeongoza hatua hiyo ndiyo bingwa wa Ligi hiyo.

Wiki ijayo Genk yenye pointi 50, itashuka tena dimbani katika mchezo wa raundi ya nane dhidi ya Club Brugge KV wenye pointi 41, kuelekea kuhitimisha Ligi hiyo kabla ya kutangazwa kwa bingwa wa msimu 2018- 2019.

Post a Comment

0 Comments