STAA wa Muziki wa Bongo Fleva kutoka katika Lebo ya WCB, Raymond Shaban Mwakyusa ‘Rayvanny’ amepanga kufanya shoo ya maana siku ya Iddi Pili katika Uwanja wa Taifa wa Burudani pale Dar Live uliopo Mbagala Zakhiem, Dar. Shoo hiyo ambayo ameipa jina la Vanny Day

 

 

kutoka Temeke kwa kumsapoti na kumuamini kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne tangu atoboe kimuziki. Akipiga stori na Championi Jumamosi, Rayvanny alisema ameamua kuipeleka shoo Dar Live kwa sababu ya ukubwa na ubora wa kiwanja hicho na kuwashukuru mashabiki wake kutoka mitaa ya Temeke kwa kumuamini na kumpa sapoti kubwa tangu alivyoachia ngoma yake ya kwanza.

 

“Nimeipeleka shoo yangu ya Vanny Day katika kiwanja cha Dar Live kwa sababu ya ubora na ukubwa wa kiwanja hicho lakini kubwa kwenda kufanya balaa na mashabiki zangu kutoka pande za Temeke ambao wamenisapoti kwa kipindi chote tangu natoboa kimuziki,” alisema Rayvanny. Aidha meneja wa burudani wa Dar Live, KP Mjomba alisema; “Dar Live hatujawahi kukosea na ndiyo maana wasanii kama Rayvanny wameichagua Dar Live kama sehemu ya kufanyia maangamizi makali ya kiburudani.”

EXCLUSIVE:”RUGE Hakuwahi kunitambulisha kwa NANDY kuwa ni MCHUMBA WAKE”/Namjua ZAMARADI – BARNABA

The post Rayvanny Apeleka Balaa Dar Live appeared first on Global Publishers.