Windows

Baada ya Bocco, Mkude na Okwi wanafuata





Simba tayari imeanza mchakato wa kuhuisha mikataba ya wachezaji wake ambayo inamalizika mwishoni mwa msimu
Baada ya kumalizana na nahodha John Bocco, inaelezwa mshambuliaji Emmanuel Okwi na Jonas Mkude wako katika mazungumzo na uongozi wa Simba ili kuhuisha mikataba yao
Wachezaji hao wanadaiwa kunyemelewa na timu nyingine hivyo kuulazimu uongozi wa Simba kuharakisha kuwapa mikataba mipya
Okwi amekuwa akihusishwa na timu kadhaa kutoka Afrika Kusini, ambapo mwezi Januari Kaizer Chiefs iliwasilisha ofa kwa klabu ya Simba lakini uongozi 'ukaipiga chini'
cut
Mkude anatajwa kuwaniwa na timu kadhaa kutoka Arabuni
Wachezaji wengine ambao wako katika mipango ya mwalimu na watasaini mikataba mipya pia
Aidha Simba huenda isifanye mabadiliko makubwa ya kikosi chake hasa kwa wachezaji wa ndani baada ya Aussems kuagiza waliopo waongezewe mikataba kwa kuwa nje ya Simba hakuna wachezaji wengi bora
Wachezaji wa ndani wanaotajwa kujiunga na Simba kwa ajili ya msimu ujao ni pamoja na Vitalis Mayanga kutoka Ndanda Fc.
Mayanga alisajiliwa kwa ajili ya michuano ya CAF lakini taarifa zake zikachelewa kutumwa
Wengine ni Ibrahim Ajib kutoka Yanga na Beno Kakolanya (huru)

Post a Comment

0 Comments