Windows

Kocha Mbao afunguka mazito



KOCHA Msaidizi wa kikosi cha Mbao, Fulgence Novatus, amesema kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa KMC kilisababishwa na wachezaji kutokuwa na utayari wa mchezo.

Mbao walipata kipigo hicho katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa Jumanne wiki hii kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini hapa.

Akizungumza na BINGWA juzi, kocha huyo alisema wachezaji wake walipambana pasipo maandalizi kwa siku mbili.

Kocha huyo alisema wachezaji hawakuwa tayari kucheza, hivyo walistahili kufungwa.

Alisema akili za wachezaji hazikuwa tayari kwa kucheza mchezo wa ushindani.

“Jambo muhimu ni kuwa kama wamekubali kucheza leo (Jumanne), basi tunaamini mechi ijayo watakuwa bora zaidi,” alisema.

Kwa matokeo hayo Mbao FC wanashika nafasi ya 13 kutokana na pointi 44, baada ya kucheza michezo 37 wakisaliwa na mmoja dhidi ya Kagera Sugar.

Alisema mchezo huo utaamua hatima yao ya kubaki Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Hata hivyo, alisema sababu nyingine ya kufanya vibaya mchezo huo, ilitokana na mgomo wa wachezaji walioshinikiza malipo yao.

Alisema licha ya uongozi kutatua mgomo wa wachezaji kabla ya mchezo huo, lakini waliingia dimbani wakiwa hawana utimamu wa akili na mwili.

Post a Comment

0 Comments