Windows

RASMI SIMBA SASA KUMENYANA NA SEVILLA KUTOKA HISPANIA, TFF YATAJA SABABU

IMEELEZWA kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania, Simba watamenyana na kikosi cha Sevilla ambao ni Mabingwa mara tano wa UEFA kutoka nchini Hispania ambacho kinashiriki La Liga.

Mchezo huo wa kihistoria unatarajiwa kuchezwa Mei 23 Uwanja wa Taifa Dar ambapo Sevvila watakuwa kwenye ziara ya kimichezo ya siku tatu inayokwenda kwa jina la 'La Liga World SportPesa Challenge' inayodhaminiwa na kampuni ya kubashiri ya SportPesa.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania Abbas Tarimba amesema kuwa hilo ni lengo la kukuza na kuboresha michezo Tanzania.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wlilfred Kidao amesema kuwa sababu ya kuichagua Simba kumenyana na Sevilla ni kutokana na timu hiyo kumaliza ikiwa nafasi ya tatu kwenye michuano ya SportPesa Super Cup ikiwa ni nafasi ya juu zaidi kwa timu za Tanzania.


Post a Comment

0 Comments