Windows

BREAKING NEWS: SIMBA KUWAVAA VIGOGO WA HISPANIA DAR, NI SEVILLA, INATANGAZWA LEO





Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeipitisha Simba kuwavaa moja ya vigogo wa Ulaya, Sevilla.

Sevilla ni moja ya kikosi bora barani Ulaya kutoka nchini Hispania na kinatarajia kuwa na ziara nchini, mwishoni mwa Mei.

Habari kutoka ndani ya TFF, zimeeleza kuwa shirikisho hilo limetoa nafasi kwa Simba kutokana na kuwa mabingwa watetezi lakini waliokuwa wawakilishi wa Tanzania waliofika robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Sevilla inaletwa nchii na wadhamini wakuu wa Simbana Yanga, kampuni ya kubeti ya SportPesa ambayo sasa ni kampuni maarufu zaidi ya michezo hiyo nchini.


Post a Comment

0 Comments