Windows

YANGA YAFICHUA KILICHOIPONZA AZAM FC KUPIGWA JANA UWANJA WA UHURU

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kilichoiponza timu ya Azam FC kupoteza mchezo wa jana ni kutumia nguvu nyingi uwanjani hali iliyowafanya wakapoteza nafasi walizotengeneza.

Kwenye mchezo uliochezwa jana uwanja wa Uhuru, Azam ilifungwa bao 1-0 na Yanga lililopachikwa na Mrisho Ngassa dakika ya 13.

Akizungumza na Saleh Jembe, Zahera amesema kuwa alikisoma kikosi cha Azam namna kinavyocheza na mbinu zake hali iliyomfanya kuunda kikosi cha ushindi mapema.

"Nilikiandaa kikosi kwa muda kidogo hasa baada ya kufuatilia Azam FC, ni timu nzuri ina wachezaji wazuri ila wanashindwa kutulia na kutumia akili, hapo ndipo niliwaweza na baada ya bao kuingia waliongeza matumizi ya nguvu.

"Utaona namna wachezaji wangu walivyokuwa wakidondoka sababu haikuwa kuchoka ilikuwa ni nguvu za wachezaji wa Azam FC, ila kama wangetumia akili ulikuwa mchezo mgumu kwangu," amesema Zahera.

Uhindi huo unaifanya Yanga kujikita kileleni na pointi zake 77 baada ya kucheza michezo 33 na kubakiwa na michezo mitano.

Post a Comment

0 Comments